USHAURI NA UNASIHI
USHAURI
Nini maana ya ushauri
Ni matumizi ya ujuzi ulionao kwa makundi kwa kuwasaidia watu wengine kuweza kugundua au, kutekeleza masuluhisho katika matatizo yao.
- Katika mazungumzo hayo mshauriwa anapaswa kujihisi yupo salama, kwa sababu ushauri huwa unahusisha utaratibu wa kuwasaidia watu waweze kutatua matatizo yao wenyewe.
- NI mazungumzo kati ya mtu mwenye ujuzi utaalam na uzoefu wa kusikiliza na kutoa mwongozo wa namna ya kutatua tatizo la mtu ama kikundi cha mtu.
- Ushauri unahitaji watu wawili au zaid
MAMBO YANAYOHITAJI USHAURI
- Uchaguzi wa marafiki
- Uchaguzi wa makundi mbalimbali ya kujisomea
- Uchaguzi wa Muda
- Uchaguzi wa masomo
- Kubadili tabia. N. K
UNASIHI
Nini maana ya unasihi
Ni kitendo cha kumsaidia mtu, kutambua matatizo yake na kuwa t
ayari kubadilika
Tofauti kati ya Ushauri na unasihi
- Ushauri mtu anakuwa amesomea lakini Unasihi unafanywa na mtu yeyote
- Ushauri haumchagulii mtu kitu cha kufanya lakini Unasihi unamchagulia kitu cha kufanya
- Ushauri hufanywa kwa majadiliano lakini Unasihi hufanywa kwa maelekezo
- Ushauri hufanyika sehemu maalum lakini Unasihi hufanyika popote
USHAURI NA UNASIHI
Ni huduma inayotolewana mtu binafsi au, taasisi ambavyo, inajumuisha majibizano ya pande mbili kati ya mhudumu na muhudumiwa na ina lengo, la kumshauri
KANUNI ZA USHAURI NASAHA
- Msiri
- Ucheshi
- Ujuzi
- Uaminifu
- Heshima
SIFA ZA MSHAURI NASAHA
- Msikilizaji mzuri
- Matumizi ya lugha
- Ujuzi
- Awe na heshima
- Awe mwaminifu na mkweli
- Awe msiri
- Awe na utu na anaependa watu
HITIMISHO
Je upo tayari kwa ushauri na unasihi? Ipi changamoto yako? Je unachangamoto inayokutatiza au, labda unahitaji mafunzo na ushauri binafsi wa hatua kwa hatua ili uweze kushindana na hali uliyonayo?
0 Comments